Zuma kulipa Dola 500,000 katika kashfa ya makazi yake - LEKULE

Breaking

28 Jun 2016

Zuma kulipa Dola 500,000 katika kashfa ya makazi yake

media
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akijibu maswali mengi ya Wabunge na Maseneta kuhusu kesi inayojulikana kama "Gupta" inayoibua maswali mengi katika utawala wake.
Jumatau hii Juni 27, Wizara ya Fedha ya Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Katiba ya Afrika Kusini imemuamuru Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kulipa Dola 500,000 kama kitita cha pesa kiliyotumiwa kinyume cha sheria katika kashfa ya makazi yake binafsi ya Kandla.
"Jumla ya kitita ambacho Rais Zuma anapaswa kulipa ni sawa na Rand 7814555", sawa na sehemu ya kazi iliyofanyika katika ujenzi wa makazi yake kwa matumizi ya fedha za umma, mamlaka ya Hazina ya taifa imebaini kwenye stakabadhi iliyokabidhiwa Mahakama ya Katiba.
Juma lililopita Mahakama nchini Afrika Kusini ilitupilia mbali jaribio la Rais Jackob Zuma, kukata rufaa kupinga hukumu iliyoagiza afunguliwe mashtaka ya rushwa zaidi ya 800.
Rais Zuma alijaribu kupindua uamuzi wa awali wa mahakama wa mwezi Aprili, ya kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka ifungue upya mashtaka ya rushwa dhidi yake, yaliyofutwa mwaka 2009, siku chache kabla ya kuwa Rais.
Mashtaka dhidi ya Rais Zuma yanahusu rushwa, udanganyifu, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya fedha za uma, kuhusu ununuzi wa silaha za kijeshi uliogharimu mabilioni ya dola za Marekani.
Rais Zuma amekuwa akipamabana kusafisha jina lake kutokana na tuhuma kadhaa za rushwa zinazomkabili, sambamba na ukosolewaji mkubwa kuhusu sera ya ajira nchini humo.
Mwaka 2009, ofisi ya mwendesha mashtaka ilitoa maelezo ya kwanini ilimuondolea Rais Zuma mashtaka zaidi ya 700 ya rushwa, ikisema mawasiliano yaliyonaswa wakati wa utawala wa rais Thabo Mbeki hayakuwa na uhusiano wowote kwenye kesi ikiwa wangefungua mashtaka.
Uamuzi huu wa ofisi ya mwendesha mashtaka, ulisafisha njia kwa Rais Zuma, kiongozi wa chama tawala nchini humo cha ANC, kuwania urais wiki chache baadae.
Mawasiliano yaliyorekodiwa ambayo yalifahamika kama "Spy tapes" yalifanywa kuwa siri, hadi pale yalipowekwa wazi mwaka 2014 baada ya muda mrefu wa ushindani wa kisheria mahakamani, kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance. RFI

No comments: