Wakimbizi 50,000 wa kisomali kuondoka Dadaab - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Monday, 27 June 2016

Wakimbizi 50,000 wa kisomali kuondoka Dadaab


Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya
Shirika la kuhudumia wakimbizi nchini Kenya limesema wakimbizi 50,000 wa kisomali wanaoishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab watarejea makwao kwa hiyari mwishoni mwa mwaka huu.
Shirika hilo limesema kila mkimbizi atakayerejea atapatiwa dola za marekani mia mbili pia msaada wa chakula na matibabu kwa kipindi cha mpaka miezi tisa.
Mamlaka za Kenya zimesema zinataka kufunga kambi, hasa ambazo zinawatunza wasomali.
Mamlaka hizo zimesema zitawahamisha wakimbizi wa kutoka Sudani Kusini na kuwapeleka kwenye Kambi nyingine.
Idadi ya wakimbizi kambini Dadaab huenda ikapungua mpaka kufikia watu laki moja na nusu mwishoni mwa mwaka.BBC
Post a Comment