Wahariri wakamatwa Zambia - LEKULE

Breaking

29 Jun 2016

Wahariri wakamatwa Zambia



Gazeti la The Post linadaiwa kuwa na deni la kodi ya mamiilioni ya dola

Polisi nchini Zambia imemkamata Mhariri wa Gazeti kuu nchini humo,sambamba na mke wake pamoja na naibu Mhariri mtendaji.
Juma lililopita mamlaka nchini humo ililifungia Gazeti la The Post ikisema linadaiwa kodi ya mamilioni ya Dola.
Uongozi wa gazeti hilo unadai kuwa hakuna kodi inayodaiwa na serikali huku wakitaja kitendo hicho kuwja aribio la kutaka kuzuia uhuru wa habari wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi wa nane.
Watu hao watatu walikamatwa walipoingia katika ofisi kuu za gazeti hilo mjini Lusaka.Pamoja na mashtaka mengine, wanatuhumiwa kufanya uhalifu.BBC

No comments: