Maamuzi ya kocha wa England baada ya kutolewa Euro 2016 - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 28 June 2016

Maamuzi ya kocha wa England baada ya kutolewa Euro 2016Siku ya June 27 2016 huenda ikawa ni siku ambayo mashabiki wa soka wamepata habari ambazo huenda hawakuzitarajia kutokana na matokeo ya mechi zenyewe, tulianza kusikia taarifa za Lionel Messi, Aguero na Javier Mascherano wakitangaza kustaafu kutokana na kupoteza mchezo wao wa fainali ya Copa America dhidi ya Chile.
Kama ambavyo Messi na wenzake wamefanya, kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hogdson ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa England, kutokana na kupoteza mchezo wao wa 16 bora dhidi ya Iceland kwa kufungwa goli 2-1, England walianza kupata goli la uongozi dakika ya 4 kupitia kwa Wayne Rooney.
Dakika mbili baadae baada ya England kupata goli la uongozi, Iceland walisawazisha kupitia kwa Ragnar Sigurdsson dakika ya 6 na Kolbeinn Sigposson dakika ya 18. Roy Hodgson ametangaza uamuzi huo wa kujiuzulu kuendelea kuifundisha England, ikiwa ni siku tatu zimebakia mkataba wake umalizike.
Post a Comment