Unakumbuka ujenzi wa gorofa la mamilioni chini ya kiwango Dsm? Mwanasiasa amefikishwa Mahakamani leo - LEKULE

Breaking

6 Apr 2016

Unakumbuka ujenzi wa gorofa la mamilioni chini ya kiwango Dsm? Mwanasiasa amefikishwa Mahakamani leo



Ujenzi wa majengo ya ghorofa yaliyo chini ya kiwango yaliripotiwa katika jiji la Dar es salaam miaka ya nyuma iliyopita ambapo kariakoo kulikuwa na ghorofa 64, taarifa nyingine ilikuwa ni ya jengo la ghorofa kuporomoka na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
April 06 2016 Bodi ya Wakandarasi imemfikisha Mahakamani Kisutu Dar es salaam mfanyabiashara na Mwanasiasa Thomas Ngawaiya kwa kosa la kufanya shughuli za ujenzi wa jengo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya MILIONI 500 Kinondoni Dar es salaam bila kutumia wakandarasi waliosajiliwa.
Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ambayo amedhaminiwa na wadhamini wawili ambapo masharti yake kila mmoja awe na ahadi ya  MILIONI 250 na hati ya nyumba. 
Akizungumza baada ya kesi hiyo Mwanasheria wa Bodi ya usajili wa makandarasi, Saddy Kambona amesema….>>>’Mtuhumiwa ameshtakiwa kwa kutokutumia wakandarasi waliosajiliwa kama ambavyo sheria ya bodi ya makandarasi namba 17 ya 1997 na ilipofanyiwa 2008 inavyotaka kwamba majengo yote ya matumizi ya umma lazima yajengwe kitaalamu na wakandarasi waliosajiliwa kwa hiyo shughuli hizo za ujenzi zimekuwa zikiendelea bila kuwepo kwa wakandarasi waliosajiliwa badala yake umekuwa unafanywa na mafundi wa kawaida tu’.

No comments: