Rais Magufuli ametoa shilingi Milioni 10 nyumbani kwao Geita leo - LEKULE

Breaking

3 Apr 2016

Rais Magufuli ametoa shilingi Milioni 10 nyumbani kwao Geita leo



President John Pombe Magufuli wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania yupo nyumbani kwao chato kwa mapumziko ya siku tano ambapo toka ateuliwe kuwa Rais wa Tanzania, hii ni mara yake ya kwanza kwenda Chato.
Taarifa za Jumapili ya April 3 2016 Rais Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa la bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchagia upanuzi wa kanisa hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.
Kabla ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao unaendelea.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia kuadhimisha miaka 50  tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao unachangiwa na waumini wenyewe.
Padre Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.

No comments: