RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA VITI MAALUUM WA CHADEMA JIJINI DAR LEO - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 13 April 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA VITI MAALUUM WA CHADEMA JIJINI DAR LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, wakati walipowasili kwenye viwanja vya Karimjee, kulikofanyika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mkewe Mama Jannet Magufuli, wakisalimiana na baadhi ya waheshimiwa wabunge waliokuwepo kwenye shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa pole, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, kufuatia msiba wa Mbunge wa Chama chake, Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukuwasili kwenye ukumbi wa Karimjee leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, akifuatiwa na Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.

 Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Veronica Mallya akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akiagana Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.


Post a Comment