NMB yatoa neema kwa Hospitali na vituo vya Afya Nchini - LEKULE

Breaking

14 Apr 2016

NMB yatoa neema kwa Hospitali na vituo vya Afya Nchini


Benki ya NMB leo imesaini makubaliano na shirika lisilo la kiserikali la STICHTING MEDICAL CREDIT FUND (MCF) la nchini Uholanzi kwaajili ya kutoa fursa za mikopo nafuu kwa hospitali, vituo vya Afya na maduka ya dawa nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora na nafuu za afya nchini.

Mkopo huu utatolewa kwa hospitali za binafsi (zisizo za serikali) ambapo hospitali na vituo vya afya vitaweza kukopa kuanzia shilingi milioni 30 mpaka bilioni 2.

NMB inategemea kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mengi zaidi nchini tofauti na sasa ambapo hospitali nzuri zinazotoa huduma bora zinapatikana sehemu chache. NMB itatoa mikopo kwaajili ya uwekezaji zaidi kwenye sekta ya afya huku MCF watatoa elimu juu ya usimamizi wa utoaji huduma na upatikanaji wa vifaa bora katika sekta ya Afya.

NMB inakuwa benki ya kwanza nchini kuingia ubia na MCF taasisi ambayo tayari inafanya kazi zake nchini Kenya, Nigeria na Ghana.
MCF wamechagua kufanya kazi na NMB kutokana na ukweli kwamba benki hiyo ina mtandao mpana wa matawi nchi nzima kuliko benki yoyote hivyo kurahisisha utoaji wa huduma kwenye maeneo mengi zaidi hata vijijini.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlwsvqay421i0MnPE4AUisBvxpPhq4yR2nAIJvSoGfZ4TtNchW-8rDW-993Vnf5v_3LSPQpjY_aDBiI_K2xdmPG0Z3JDWgmeDdurhIUoSGlYIJJR7qmevnx3MdqXkjzWup8818N7lDJFw2/s1600/MOU+PIC+1.jpgAfisa Mtendaji Mkuu wa Medical Credit Fund (MCF)- Bi Monique Dolfing-Vogelenzang (kushoto) na Mkurungenzi Mtendaji wa NMB - Bi Ineke Bussemaker wakisaini makubaliano yatakayowezesha sekta ya afya kupata mikopo nafuu kutoka NMB. Nje ya mikopo, MCF itasaidia kutoa elimu juu ya usimamizi wa utoaji huduma na upatikanaji wa vifaa bora katika sekta ya Afya.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgh2wDInrTu7S73Rh3fcToopi5RB3aqymSTVkXevcZNvKnxsOcqd_7HdwTJy7eIPyovDbR4IsCmP7-j_HgV4FvhGcvfhsxn40h99L7wIfeAVQWYrGP6reiypblHgBzcUVaiTzgG8hvX82wV/s1600/MOU+PIC+2.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTrSu6mFFROTunss_YUsVyTLpV6-EQbk9VOCUG5FAlq7uz1R5kNWJbwC_mLcrz3Gee9D-IQjIpvauMGreCKR2khYrUTMd22LQjYpuW6s5Cnrnx8aUd34R4587GHIXBWna0AcrymV2quw03/s1600/MOU+PIC+3.jpg


Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Abdulmajid Nsekela akiongea na waandishi wa habari juu ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya NMB NA MCF kwaajili ya utoaji wa mikopo nafuu kwenye sekta ya afya hususani hospitali, vituo vya afya na maduka ya dawa ya binafsi.

No comments: