Mvutano wa Tanzania na Kenya kwenye ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda umezungumziwa - LEKULE

Breaking

29 Mar 2016

Mvutano wa Tanzania na Kenya kwenye ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda umezungumziwa



Wakati Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga ukitarajiwa kuanza baada ya hatua mbalimbali za mazungumzo kukamilika, taarifa zilizotoka March 28 2016 ni kwamba huu mradi umeziingiza Tanzania na Kenya kwenye mvutano.
Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini Prof Justin Ntalikwa amekiri kuwepo kwa mvutano ila ametoa uhakika wa asilimia 98 kwa Tanzania kuuchuka mradi huo >>>’kwanza tuna uzoefu mkubwa katika ujenzi wa haya mabomba, tuna mabomba kama manne hivi ambayo tayari tumeshayajenga, uwepo wa bandari ya kina kirefu iliyopo Tanga ambayo inaweza kuchukua meli mbalimbali ambazo zinakuja kuchukua hayo mafuta, vilevile nchi yetu ina usalama zaidi ikilinganishwa na hao wenzetu tunaoshindana nao’
Kingine alichothibitisha ni kwamba wamekutana na wafanyabiashara ili kujadili ni jinsi gani wafanyabiashara hao wanaweza kuchangia katika kuchukua fursa mbalimbali zitakazojitokeza baada ya kuupata mradi wa ujenzi wa bomba la  mafuta ghafi unaotarajiwa kujengwa.
>>>‘kwenye huo mradi kuna fursa ambazo ni pamoja na kupata tenda mbalimbali katika kazi zitakazojitokeza,  ajira zitakazoweza kupatikana kwa ajili ya watu wetu Tanzania na pia kuna kodi mbalimbali zitapatikana kwa kulipwa kupitia huo mradi

No comments: