Mpya za Rais Magufuli kwenye uongozi wa TRA na TAKUKURU - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 13 March 2016

Mpya za Rais Magufuli kwenye uongozi wa TRA na TAKUKURU


Taarifa ambayo imetolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mawasiliano, IKULU Gerson Msigwa imesema kwamba  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.
Waliothibitishwa ni Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye sasa ni anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA naValentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).
Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016
Post a Comment