MBARAWA AKAGUA KIVUKO CHA KILOMBERO - LEKULE

Breaking

13 Mar 2016

MBARAWA AKAGUA KIVUKO CHA KILOMBERO


1
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  akishuka kwenye kivuko cha MV KILOMBERO mara baada ya kukikagua.
2
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  katikati akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan kulia na mkuu wa wilaya ya Kilombero Lephy Gembe kushoto wakati akikagua kivuko hicho mara baada ya ukarabati.
3
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  akishuka kutoka katika kivuko cha Mv Kilombero mara baada ya kukagua utendaji kazi wa Nahodha wa kivuko hicho.
4
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  akitoa maelekezo kwa wakazi wa wilaya za Kilombero na Ulanga kuhusu umuhimu wa kulipa nauli ya kivuko na kuzingatia usalama wawapo kwenye kivuko mara baada ya kukikagua kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero unakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ili kumaliza changamoto ya usafiri inakabili wanachi wa wilaya za KILOMBERO na ULANGA mkoani MOROGORO.
Prof. MBARAWA ametoa kauli hiyo Wilayani KILOMBERO mkoani MOROGORO mara baada ya kukagua maendeleo ya kivuko cha MV- KILOMBERO kilochokuwa kikikarabatiwa kufuatia kuzama mwishoni mwa mwezi Januari ambapo amesema tayari Serikali imemlipa mkandarasi zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja ili kuhakikisha ujenzi wa daraja katika mto huo linakamilika kwa wakati.
Amesema tayari mkandarasi anayejenga daraja hilo kutoka China ameshalipwa shilingi bilioni 11.2 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo hivi sasa kazi inayoendelea kwa mkandarasi huyo ni kutengeza vifaa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo huko nchini China .
“ Ifikapo novemba mwaka huu tutakuwa tumelipatia ufumbuzi wa kudumu swala la daraja la Kilombero na hivyo mpapita kwa uhakika na kufanya biashara zenu kwa uhakika”, amesema Prof.MBARAWA.
Aidha Prof. Mbarawa amekagua na kuruhusu kuanza tena kwa shughuli za usafirishaji katika kivuko cha Mv Kilombero ambazo zilikuwa zimesimama kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja tangu kivuko hicho kupata ajali mnamo Januari mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo.
Ukabati wa kivuko hicho umegharimu shilingi milioni 342.5 ambapo Prof.MBARAWA amewataka wananchi kufuata maelekezo ya wasimamizi wa kivuko wakati wa safari zao na kulipa nauli stahili.
“Lazima mlipe nauli kwa sababu nauli hiyo ndio tunayotumia kuendeshea vivuko na pia mzingatie usalama wenu na kusikiliza maelekezo ya wasimamizi wa kivuko ili kuepuka kadhia “amesisitiza Prof.MBARAWA.
Ujenzi wa daraja katika mto Kilombero ni sehemu ya mkakati wa Serikali tangu awamu ya kwanza uliolenga kujenga madaraja makubwa ni daraja la mto Rufiji mkoani Pwani, daraja Kirumi mkoani Mara, daraja la Malagarasi mkoani Kigoma na Kigamboni la jijini Dar es salam.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

No comments: