Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania - LEKULE

Breaking

31 Mar 2016

Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania



Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REALutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya fedha zote tunazofanyia kazi na  hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’
>>>’Shughuli za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.

No comments: