Kama yalikupita matokeo ya Arsenal na ya Man United FA Cup March 13, matokeo haya - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 13 March 2016

Kama yalikupita matokeo ya Arsenal na ya Man United FA Cup March 13, matokeo haya

Jumapili ya March 13 Kombe la FA nchini Uingereza limeendelea kama kawaida kwa vilabu kadhaa kushuka dimbani kucheza mechi yake ya raundi ya sita ya michuano hiyo.
March 13 michezo ya Kombe la FA Uingereza ilichezwa miwili, kwa klabu ya Arsenal kuchuana na klabu ya Watford na kuishia kuambulia kichapo cha goli 2-1.

Baada ya hapo Man United walifuatia kucheza mchezo wao wa raundi ya sita ya Kombe la FA dhidi ya wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham United, ambao nao kupitia kwa Dimitri Payet dakika ya 68 waliifunga Man United, lakini Man United walikuja juu na kuambulia sare ya goli 1-1 baada ya Anthony Martial kusawazisha goli dakika ya 83
Post a Comment