DRC: Nani alihusika na mauaji ya askari wa kulinda amani wa Tanzania Beni? - LEKULE

Breaking

6 Mar 2016

DRC: Nani alihusika na mauaji ya askari wa kulinda amani wa Tanzania Beni?

Askari wawaili wa kulinda amani kutoka Tanzania wakipiga doria nje ya mji wa Goma, Oktoba 6, 2013.
Askari wawaili wa kulinda amani kutoka Tanzania wakipiga doria nje ya mji wa Goma, Oktoba 6, 2013.

Nani alihusika na mauaji ya askari wa kulinda amani wa Tanzania mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 5, 2015? Tukio hilo bado linaibua maswali mengi hadi sasa, kwani ushahidi wa kwanza wa uchunguzi ulioendeshwa na mahakama ya kijeshi ya Congo unatofautiana na matokeo ya hivi karibuni ya wataalam wa Umoja wa Mataifa.
Wataalam hao wanabaini katika ripoti ya siri, kwamba majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC)yalihusika katika shambulio hilo la kuvizia dhidi ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO0 katika eneo la Beni. Mara tu baada ya ushahidi huo, mamlaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilianzisha uchunguzi. Jumamosi hii, Machi 5, RFI inaonyesha ushahidi wa kwanza wa ripoti ya mahakama ya kijeshi ambayo inabaini kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF-Nalu na kwamba askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) waliwasili kwenye eneo la tukio baada ya hali hiyo kutokea.
Mahakama ya jeshi katika eneo la Beniiliwahoji watu watao, wakiwemo maafisa wanne waliotumwa katika wilaya ya Beni wakati wa tukio hilo, na mtu mmoja aliyenusurika katika shambulio hilo, muendesha pikipiki ya kukodiwa.
Mashahidi hao watano, wote walikanusha ripoti ya timu ya wataalam wa Umoja wa Mataifa. Mkuu wa bataliani ya kwanza mjini Mayi Moya, karibu na eneo la shambulio, alikuwa Oicha na alisema alipokea simu akiambiwa kwamba mji wa Beni umeshambuliwa. Anasema kuwa alichukua pikipiki akiambatana na mlinzi wakewakielekea katika eneo la tukio. Kutokana na milio mingi ya risasi na baada ya kubadilishana risasi na kundi la wahalifu, aliamua kwenda kutafuta msaada.
Kwa mujibu wa ripoti hii ya utafiti na ushahidi uliotolewa, wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasadikiwa kuwa waliwasili katika eneo la shambulio baada ya mapigano na inasadikiwa kuwa waligundua miili miwili ya askari wa kulinda kutoka Tanzania na raia watatu. Pia waliokota silaha zilioachwa naaskari wa Tanzania, ambazo walizkabidhi kwa wahusika baadaye, ripoti hiyo inaeleza.
Shahidi raia aliohojiwa, yeye, anaeleza kuwa alikuwa nyuma ya msafara wa wanajeshi wa Tanzania wakati shambulio hilo lilitokea. Raia huyo aliiambia mahakama ya kijeshi ya Congo kwa shambulio hilo liliendeshwa na raia wenye silaha, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, ambao ripoti ya mahakama ya kijeshi inabainisha kuwa ni waasi wa Uganda wa ADF-Nalu.

Mwendesha mashitaka kwenye mahakama ya kijeshi pia amesema kuwa alikutana na mwakilishi wa timu ya mtaalam wa Umoja wa Mataifa. Inasemekana, kupitia ripoti hii, kwamba wataalam wa Umoja wa Mataifa pia wana mashahidi watano ambao wanathibitisha toleo lao kuhusu tukio hilo, Mashahidi hao wa wataalam wa Umoj aw aMatiafa ni mpiganaji wa ADF-Nalu, afisa wa jeshi la congo (FARDC).

No comments: