Yoweri Museveni Atashinda Uchaguzi Wa Alhamisi - LEKULE

Breaking

15 Feb 2016

Yoweri Museveni Atashinda Uchaguzi Wa Alhamisi

Ndugu zangu,
Jirani zetu Waganda wanakwenda kupiga kura Alhimisi Februari 18, 2016. Naziona ishara za Yoweri Museveni kushinda uchaguzi huo.
Kwanini?
Nina bahati ya kufuatilia kwa karibu siasa za Uganda tangu pale vikosi vya Tanzania vilipoingia Kampala na kumwondoa madarakani Idd Amin.
Kwenye Serikali za mpito akaja Profesa Kilonge Lule aliyedumu Ikulu kwa siku 68. Akaapishwa Godfrey Binaisa mwaka ule ule wa 1979. Ukafanyika uchaguzi wa kwanza wa ' maruweruwe' wa 1980 uliomwingiza madarakani Dr Milton Obote.
Mwelekeo mbaya wa Uganda ulionekana kwenye mkutano wa Moshi, Tanzania, mwaka 1979. Ni pale Waganda walipokutanishwa na Julius Nyerere wajadili mustakabali wao kwenye ardhi ya Tanzania. Museveni alikuwepo, Dr. Milton Obote alizuiwa na Nyerere asije Moshi akitokea uhamishoni Lusaka. Sababu? Nyerere alifahamu, kwenye mkutano huo uwepo wa Obote ungeharibu zaidi kuliko kujenga. Nyerere alimwambia Obote aandike tu barua ya kuutakia heri mkutano!
Uchaguzi wa ' Maruweruwe' wa 1980 ulimwingiza madarakani Obote ukawa mwanzo wa mapambano mapya ya Waganda. Waasi sasa waliongozwa na Yoweri Museveni.
Museveni akaunda NRA- National Resistance Army. Alikuwa na uzoefu wa vita vya msituni. Akaingia madarakani 1986. Miaka kumi baadae nilifika Kampala na kutembea hata maeneo ya vijijini. Niliona jinsi Museveni na NRM- Nationali Resistance Movement alivyofanikiwa kuiga mfumo wa TANU na CCM katika kutengeneza mtandao vijijini.
Tatizo la upinzani Uganda ni kama kwengineko Afrika. Umegawanyika sana na wanaogombania wametokana kwenye mfumo huo huo wanaopingana nao. Mfano, Amama Mbabazi kwa Waganda wengi wanamwona kama ' mkosaji tu'. Aliutumikia mfumo wa Museveni kwa miaka mingi hadi pale aliponyimwa nafasi ya kugombea urais kutoka chama chake.

Kuna mengi ya kuyachambua. Nitarudi tena...

No comments: