Waziri Wa Mambo Ya Nje Augustine Mahiga Ala Kiapo Bungeni Akiwa Mpweke - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 3 February 2016

Waziri Wa Mambo Ya Nje Augustine Mahiga Ala Kiapo Bungeni Akiwa MpwekeKiapo cha uaminifu cha Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga jana, kilikuwa sawa na viapo vingine, lakini alikosa vionjo kama ilivyokuwa kwa wenzake.

Mwanzoni mwa mkutano wa pili wa Bunge la 11, mawaziri na naibu mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli walikula kiapo cha utii kwa Bunge ili kutimiza majukumu yao.

Katika viapo hivyo kulikuwa na mbwembwe nyingi kutoka kwa wabunge, hasa wanawake ambao kila lilipoitwa jina la mtu walipiga kelele na kumsindikiza hadi mbele alipokuwa akiwaapishia Spika. 

Hali ilikuwa tofauti jana, wakati Dk Mahiga alipoitwa kwa ajili ya kura kiapo maana hakukuwa na mbwembwe wala vigelegele kutoka kwa wabunge na pia aliingia akiwa peke yake na mpambe wa Bunge aliyekuwa anamuongoza.

Haikujulikana ni wapi walikokuwa wabunge wa CCM ili wamshangilie waziri, jambo lililoonyesha upweke kwa upande wake, ikizingatiwa hata Waziri Mkuu hakuwa kwenye kiti chake na kiongozi wa upinzani pia hakuwapo ambao utaratibu huwapa nafasi ya kuwakabirisha wabunge wapya. 

Post a Comment