Wahamiaji: mvutano mkubwa kati ya Ugiriki na Austria - LEKULE

Breaking

26 Feb 2016

Wahamiaji: mvutano mkubwa kati ya Ugiriki na Austria

Wahamiaji wakipanga foleni kwa kusubiri wapewe chakula, katika mji wa Gevgelija kwenye mpaka kati ya Makedonia na Ugiriki Februari 24, 2016.
Wahamiaji wakipanga foleni kwa kusubiri wapewe chakula, katika mji wa Gevgelija kwenye mpaka kati ya Makedonia na Ugiriki Februari 24, 2016.

Na RFI
Mvutano mkubwa kati ya Ugiriki na Austria umeleta athari Alhamisi hii katika mkutano wa nchi za Umoja wa Ulaya mjini Brussels. Mkutano ambao unalenga kukomesha hali inayojitokeza dhidi ya ongezeko la wahamiaji. Hali hii inaweza kuzua mgogoro mkubwa wa kibinadamu.
Umoja wa Ulaya unaonyooshewa kidole na nchi kadhaa zikiongozwa na Austria umelaumiwa kwa kutolinda vya kutoosha mpaka wa nje wa Umoja huo ambapo wakimbizi wengi wamekua wakipitia kwa kuingia katika ardhi yake, Ugiriki imejibu kwa hasira wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya.
"Austria inatuchukulia kama maadui," Waziri wa mambo ya Ndani wa Ugiriki Yannis Mouzalas ameshangaa mbele ya wenzake, kwa mujibu wa chanzo cha kidiplomasia, na wakati huo huo, Athens imemuitisha balozi wake mjini Vienna kwa "mashauriano."
"Ugiriki haitokubali kuwa Lebanon ya Ulaya," Bw Mouzalas ameonya, huku akieleza kwamba wakimbizi wa Syria sasa wanawakilisha robo ya wakazi wa hiyo.
Ugiriki inahisi kweli kwamba inaendelea kujiangamiza yenyewe. Tangu mapema mwezi Januari, zaidi ya wahamiaji 102,000 waliingia nchini humo wakipitia katika bahari ya Mediterranean, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM).
Ugiriki imezidiwa kuzidiwa ikilinganishwa na mpango wa kugawanya wahamiaji wanaoomba hifadhi waliowasili katika nchi hiyo wakitokea nchi ingine za ulaya. Wakimbizi wasiopungua 600 "wameonekana" nchini Italia na Ugiriki katika miezi ya hivi karibuni kwa jumla ya 160,000 ambao wanapaswa kuwepo katika nchi hizi katika kipindi cha miaka miwili.

Na uamuzi wa Makedonia kukataa kuwapa njia raia Afghanistan kwenye mpaka wake na Ugiriki, na kuamuru raia wa Syria na Iraq kuonyesha vitambulisho vya uraia, imeiongezea Ugiriki kazi kubwa na hivo kutumbukia katika hali ya sintofahamu ya wakimbizi.

No comments: