TETEMEKO LA ARDHI: MTOTO WA MIEZI 6 AOKOLEWA - LEKULE

Breaking

8 Feb 2016

TETEMEKO LA ARDHI: MTOTO WA MIEZI 6 AOKOLEWA

Wafanya kazi za uokozi huko Taiwan, wamemnusuru mtoto wa miezi 6, kutoka kwenye kifusi cha jengo la orofa la makaazi ya watu lililoporomoka, siku moja na nusu baada tetemeko la ardhi wastani kutikisa taifa hilo.
Watu zaidi ya 170 wameokolewa, lakini zaidi ya 100 wengine bado wamenaswa kwenye kifusi cha jengo hilo katika mji wa Tainan.
Mwandishi wa BBC alioko huko, anasema watu wanaanza kuvunjika moyo, huku wakisubiri habari kuhusu jamaa zao, huku kazi ya uokozi ikiendelea kwa usiku wa pili.
Awali tabasamu ilionekana mwanamme mwenye umri wa miaka 20 alipookolewa kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka.
Runinga ya nchi hiyo ilipeperusha picha za Huang Kuang wei akiokolewa hali iliyoleta shangwe kwa familia yake na kwa waokoaji.
Makundi ya uokoaji yamekuwa yakifanya hima kuwakoa zaidi ya watu 100 walio chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka kufuatia tetemeko hilo.
Hadi sasa watu 350 wameokolewa.
Kufikia sasa inasemekana kuwa 26 ya wale waliofariki kufuatia tetemeko hilo walizikwa na majengo yaliyoharibika kabisa na kuibua swala la usalama wa majengo katika kisiwa hicho.CHANZO:BBC

No comments: