Tanzia: Msanii Wa Bongo Fleva John Woka Afariki Dunia - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 16 February 2016

Tanzia: Msanii Wa Bongo Fleva John Woka Afariki Dunia

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuimba kama mlevi, Joni Woka amefariki dunia alfajiri ya leo.

Woka amefariki baada ya juzi kupata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 
Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:
 
"Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo."

Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi. 
 
Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Post a Comment