Rwanda yasisitiza haiwezi kuwafukuza wakimbizi wa Burundi - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 11 February 2016

Rwanda yasisitiza haiwezi kuwafukuza wakimbizi wa Burundi


Luise Mushikiwabo waziri wa mambo ya nje wa Rwanda katika mkutano na wajumbe wa baraza la seneti Feb 9.2016
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo ameliambia baraza la Seneti hapo jana kwamba, Rwanda haiwezi kuwafukuza wakimbizi wa Burundi kwa muda wote hali ya wasiwasi itaendelea kuripotiwa nchini humo. Mushikiwabo amesema waliokimbilia nchini Rwanda kutoka Burundi, inamaana kuwa wanamatatizo na serikali ya Burundi, hivyo kuwafukuza nchini Rwanda mbali na kuwa ni kinyume na mila na tamaduni za Rwanda lakini pia ni kinyume na sheria za Kimataifa.
Akizungumza hapo jana Louise Mushikiwabo amesema tangu Rwanda ilipoanza kuwapokea wakimbizi kutoka nchini Burundi, kumekuwa na maswala chungu nzima ambayo yamekuwa yakiibuka, na hata ripoti nyingi zimekuwa zikitolewa, hilo ni jambo la kawaida.
Mushikiwabo amesema kinachosikitisha ni kuona badala ya kuutafutia suluhu mzozo wa Burundi, hali imekuwa ikiendelea kuwa mbaya huku ripoti zikiendelea kutolewa bila kujali madhila yanayo wakumba wananchi.
Mushikiwabo, ameendelea kukanusha madai kwamba imekuwa ikiwasaidia wapinzani wa rais Nkurunziza kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi vijana wanaokabiliana kuipindua serikali iliopo sasa nchini Burundi.
Hivi karibuni ripoti iliovuja ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa serikali ya Rwanda inawapa mafunzo vijana waliokimbilia nchini Rwanda na ambao wanajiandaa kuishambulia serikali ya rais Nkurunziza.
Mushikiwabo amesema tatizo kubwa lililopo ni kuendelea kupuuzia mzozo, vinginevyo kuna uwezekano wa kuupatishia suluhu mzozo uliopo ili kuepukana na lawama za kila wakati.CHANZO:RFI
Post a Comment