Polisi Watatu Wasimamishwa Kazi Kupisha Uchunguzi wa Binti wa Kitanzania Kuvuliwa Nguo India - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 5 February 2016

Polisi Watatu Wasimamishwa Kazi Kupisha Uchunguzi wa Binti wa Kitanzania Kuvuliwa Nguo India


Polisi watatu wamesimamishwa kazi kwa muda mjini Bangalore nchini India kwa tuhuma za kukataa kusikiliza na kupokea malalamiko ya watu walioshambuliwa na kundi la watu ambapo mwanafunzi mmoja wa kike kutoka Tanzania alivuliwa baadhi ya nguo zake. 

Polisi wamesema pia wamekamata watu wanne zaidi kuhusiana na shambulio hilo, na kufikisha idadi ya waliokamatwa kufikia tisa. 

Kundi la watu lilimshambulia na kumvua nguo mwanamke mwenye umri wa miaka 21, baada ya gari la mwanafuzi kutoka Sudan kumgonga na kumuua mwanamke mmoja wa Kihindi. 

Tukio hilo limetokea eneo la Hessarghatta siku ya jumapili. Eneo hilo lina vyuo kadhaa ambapo kuna idadi kubwa ya wanafunzi kutoka Afrika, wakiwemo 150 kutoka Tanzania.
Post a Comment