Mbunge Zimbabwe avunja rekodi ya busu Afrika - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Monday, 15 February 2016

Mbunge Zimbabwe avunja rekodi ya busu Afrika

Image captionMbunge Joseph Chinotimba Zimbabwe
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika.
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.
Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''
Image captionBwana Chinotimba na mkewe Vimbai
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.
Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.
Post a Comment