Makamishna Wawili Kati Ya Sita Wa Tume Ya Uchaguzi Zanzibar Wamepinga Uchaguzi Wa Marudio ZanzibarWakati wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa wakipinga kile kinachoendelea Zanzibar, nao makamishna wawili wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Nassor Khamis Mohamed na Ayoub Hamad wameibuka na kupinga uchaguzi huo wa marudio.

Wakizungumza na wandishi wa habari mjini Dar es salaam leo, makamishna hao wamesema kuwa sababu kubwa ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na kuvurugwa kwa katiba ya zanzibar tangu tukio la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa oktoba 25, mwaka jana.

Makamishna hao wa ZEC, wakizungumza kwa hisia na kujiamini, wamesema kuwa mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jeche hakuwa na mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi huo bila kuwashirikisha makamishna wa tume hiyo.

Tayari, Jecha ametangaza kuwa uchaguzi wa marudio utafanyika siku ya Jumapili, Machi 20, mwaka huu. Lakini wajumbe hao wa ZEC, kwa pamoja wamesema wanapinga kufanyika kwa uchaguzi huo kutokana na ukiukwaji wa katiba:

“Tunapinga marudio ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Machi. Uchaguzi huo si halali kulingana na matukio yaliyotokea tangu kufanyika kwa uchaguzi halali wa Oktoba 25, mwaka jana,” walisema makamishna hao wanaowakilisha CUF ndani ya ZEC.

Wamesema kuwa sababu nyingine inayowafanya kupinga uchaguzi wa marudio ni kutokana na kukamilika kwa uchaguzi wa mwaka jana ambapo uchaguzi huo ulikuwa umekamilika na baadhi ya washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani walishakabidhiwa vyeti vyao.

Wamesema kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi billion saba hadi kukamilika kwake ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi, kwani uchaguzi Zanzibar ulishafanyika na kinachoendelea ni mbinu za kuubatilisha.

Wamesema kuwa tukio la kufutwa kwa uchaguzi huo lilitanguliwa na matukio kadhaa ambayo yalionyesha wazi kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kinamshauri Jecha, na sio maamuzi ya tume yote nzima.

“Tarehe 26 october mwaka jana CCM walileta barua ya malalamiko na kumtaka mwenyekiti na tume kufuta uchaguzi huo wakati tayari tulishaanza kutoa vyeti kwa washindi.

“Baada ya hapo mwenyekiti aliitisha kikao cha tume na tuliamua kwa pamoja kuwa maombi ya CCM hayakuwa na mashiko hivyo mchakato uliendelea.” amesema Nassor Khamis mmoja wa makamishna wa tume hiyo.

Amesema kwamba baada ya maamuzi hayo ya tume, ndipo siku iliyofuata Jecha (Mwenyekiti wa Tume), hakufika katika ujumuishaji wa matokeo kwa siku nzima na baadaye walisikia tu kuwa ametangaza kufuta uchaguzi bila kuwashirikisha wajumbe wengine wa tume.

Nassor amesema: “Baada ya hapo ndipo ofisi yetu ilianza kuzungukwa na wanajeshi na kuamuriwa tusifanye lolote huku Jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar, naye akiwa amekamatwa na kupelekwa polisi.”

Wajumbe hao, wamesema kwa matukio kama hayo wanaamini kuwa tume hiyo imeacha kufanya kazi zake kisheria na sasa inafanya kazi kisiasa, jambo ambalo linampotezea sifa mwenyekiti wake kuendelea kuiongoza tume hiyo.

Aidha, wamesema kuwa hali iliyopo ndani ya tume kwa sasa sio hali ya kawaidia kuweza kusimamia uchaguzi wa haki kutokana na wajumbe wake kupingana hovyo hovyo:

“Wajumbe wamekuwa wakipingana kwa kila hoja inayoletwa…jambo ambalo linafanya uchaguzi wa marudio kutiliwa mashaka na wajumbe wengi wa tume hiyo,” amesema wajumbe hao.

Makamishna hao wamesema kuwa wametoa wito kwa wajumbe wengine wa ZEC, kuacha kufuata mkumbo na kuamua kusimamia sheria inavyosema, ili kuwapatia wazanzibar haki yao ya kikatiba..
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF