Hello

Welcome lekule blog

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation.
together in the world. #lekule86
Join us on

Lowassa Afunguka........Asema Kuitwa FISADI Kulimfanya Ajiondoe CCM Na Kuhamia ChademaAliyekuwa mgombea urais wa Chadema chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema kusakamwa kwa maneno ya kejeli, vijembe na vitisho, kuitwa gamba na fisadi ndani ya CCM ndiko kulikomfanya kukihama chama hicho na kwenda upinzani.

Lowassa aliyekuwa na nguvu ya ushawishi ndani na nje ya CCM, alihamia Chadema baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kumsaka Rais wa Tanzania, katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Lowassa alisema licha ya kuitumikia CCM kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1977, chama hicho kiliamua kutumia watu kumsakama kwa kila aina ya maneno jambo lililomfanya achoke na kuamua kuondoka.

“Nakifahamu Chama cha Mapinduzi, nakiheshimu kwani ndicho kilichonilea, lakini, kwa hali tuliyokuwa tumefikia, inafika mahali unasema imetosha,” alisema Lowassa.

Alitaja sababu nyingine iliyomfanya kuihama CCM kuwa ni kutaka mabadiliko na aliamini mabadiliko ya kweli yatapatikana nje ya chama hicho tawala na akisema hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema mabadiliko yatatafutwa hata nje ya CCM.

Alisema kwa namna yoyote, kamwe hana mpango na hawezi kurudi CCM na akasema jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ni kuijenga Chadema ambayo yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu.

“Sina mpango na wala siwezi kurejea CCM, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, na jukumu lililoko mbele yangu ni kukijenga na kukiimarisha chama changu hiki kiwe imara tangu katika ngazi ya matawi,” alisema na kuongeza kuwa kazi iliyoko mbele yake sasa ni kukiimarisha chama hicho na wamejipanga kuzunguka nchi nzima kufanya kazi hiyo pamoja na kuwashukuru nwananchi kwa imani waliyoionyesha kwake na chama chake.

Lowassa alidai kuwa kama si kura kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Alisema kazi nyingine kubwa waliyonayo sasa ni kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na Tume ya Uchaguzi inaundwa upya kwani iliyopo si huru hata kidogo.

Alisema kama isingekuwa busara na ukomavu waliouonyesha Ukawa, basi hata hali ya siasa Tanzania Bara isingelikuwa shwari kama ilivyo sasa.

“Mara baada ya matokeo ya uchaguzi, niliwashauri vijana watulie, wasifanye fujo, nashukuru walinisikiliza.”

Alisema katika uchaguzi huo yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

“Nilishinda na Ukawa ilishinda, kilichotokea kura zilichakachuliwa kwa kiasi kikubwa… wao wanajua, Watanzania wanajua na kila mtu anajua, tulishinda kwa kura nyingi sana na tulipokonywa ushindi wetu,” alisema.

Vijana wa Chadema kukamatwa 
Alisema miongoni mwa mambo yanayomuumiza na ambayo hatayasahau katika uchaguzi huo ni kitendo cha polisi kwa maagizo ya watendaji wa Serikali kuwakamata vijana waliokuwa wanakusanya matokeo na kuwadhalilisha ikiwa ni pamoja na kuwaweka mahabusu.

Alidai kuwa kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvuruga kituo chao walichokuwa wakijumuisha matokeo na kuacha kile cha CCM kilikuwa kibaya na kilichoonyesha wazi kuwa hawakuwa tayari kukubali kuona wakishindwa.

Alisema: “Ni aibu kubwa kwa Serikali kuwaumiza na kuwaweka ndani vijana wadogo wasiokuwa na hatia eti kwa sababu tu walikuwa wakiunga mkono mabadiliko."

 Uhuru wa NEC 
Lowassa alisema miongoni mwa mambo yanayozorotesha chaguzi nchini ni NEC ambayo alisema siyo huru na badala yake ni chombo kinachotumika na watawala.

Alisema chombo hicho hakitendi haki na kwamba ingekuwa mamlaka yake baada ya uchaguzi kwisha angekiondoa madarakani.

Alisema wakati umefika kwa Watanzania kuungana kudai Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi kwa maelezo kuwa bila Katiba mpya na tume huru kamwe hakuwezi kufanyika uchaguzi ulio huru na wa haki.

Demokrasia bungeni 
Akizungumzia mwenendo wa Bunge, alisema linakwenda vizuri lakini ni mapema kulizungumzia kwa sasa.

“Katika Bunge hili wameingia vijana madhubuti bungeni, lakini hatua ya Serikali kuzuia Televisheni ya Taifa (TBC) kurusha matangazo ya Bunge moja kwa moja, hiyo ni dalili ya kuminya demokrasia.”

Alisema ni aibu kubwa kwa Serikali kutumia polisi kuingia ndani ya Bunge badala ya kujenga hoja na akasema hali hiyo ikiachwa ikaendelea italitia aibu Taifa.

Alisema moja ya mambo yaliyohimizwa na ambayo Watanzania waliachiwa na Mwalimu Julius Nyerere ni utaratibu wa kujenga hoja na kutumia nguvu ya kushinda na akaongeza kuwa kitendo cha polisi kuingia na kupiga wabunge ni kuminya na kudidimiza demokrasia.

“Tanzania tunasifika duniani kote kwa kuheshimu na kufuata demokrasia, lakini Serikali imeamua kutumia polisi kuminya demokrasia, hii ni aibu kubwa kwa Taifa… Watanzania tukiacha demokrasia ikaminywa tutalitia aibu Taifa,” alisema.

Shukrani kwa Watanzania 
Lowassa anasema licha ya kupokonywa ushindi, anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata kutoka kwa Watanzania walio wengi ambao walimuamini na kumuunga mkono.

“Watanzania waliniunga mkono kwa wingi sana, hali ile ilinipa faraja kubwa…nilifarijika pia nilipowaomba watulie wakanielewa na kutulia… nawashukuru sana Watanzania walionielewa na kutulia,” alisema.

Alitoa wito kwa Watanzania kuilinda amani ya nchi huku akisema anasubiri Rais Magufuli kutimiza siku 100 ndipo atoe tathmini yake kuhusu utawala wake.

“Marais wanapimwa kwa siku 100, nasubiri siku hizo, nitasema.”

Hali ya kisiasa Zanzibar 
Akizungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kutangaza kurejewa uchaguzi upya, Lowassa alisema suala hilo ni zito na gumu na linahitaji maombi maalumu na umakini wa hali ya juu katika kulitatua.

Alitoa wito kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Magufuli kulishughulikia suala hilo mapema kabla ya Machi 20.

“Wasikubali tufike pabaya. Bado naamini tunaweza kulimaliza kwenye meza,” alisema na kuongeza:

 “Nawasihi sana viongozi hawa wasilipuuze hili suala, jambo hili likiendelea litaleta shida kubwa kwa nchi yetu, magaidi wanaweza kulitumia na kuleta madhara makubwa, wasisubiri kufika pabaya, waanze kulishughulikia sasa.”

Alitoa wito pia kwa wanaoshughulikia suala hilo kuvishirikisha na vyama vingine badala ya kulifanya kuwa ni suala la CCM na CUF pekee.

Alisema ni imani yake kuwa Watanzania ni wamoja na hakuna mtu wa kuwagawa kwa namna yoyote na kuwa wasikubali uchaguzi huo wa marudio kuwa sababu ya kuivuruga amani ya nchi

Share this:

ABOUTME

Hi all. This is deepak from Bthemez. We're providing content for Bold site and we’ve been in internet, social media and affiliate for too long time and its my profession. We are web designer & developer living India! What can I say, we are the best..

Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Labels

EDITORIALS ARTICLES LEKULE TV DC ROBOTICS DIGITAL SEMICONDUCTORS GENERATOR AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING REFERENCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT TRANSDUCER & SENSOR VIDEO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE TEARDOWN SYNCHRONOUS GENERATOR DIGITAL ELECTRONICS ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES AUTOMOTIVE MICROCONTROLLER SOLAR PROTECTION DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY WEARABLES COMMUNICATION GENERATION BATTERIES FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE CONTROL SYSTEM NUCLEAR ENERGY SMATRPHONE FILTER`S POWER BIOGAS BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS ENERGY SOURCE PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR HOME AUTOMATION 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD BLUETOOTH C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY COMPUTER DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS USB ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE APPS & SOFTWARE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS CONTROL MOTION ELECTRICAL LAWS INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RECTIFIER AND CONVERTERS RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS DC MOTOR DRIVES ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS WIRELESS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION INDUSTRIAL DRIVES LAPTOP SCIENCE THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART oscilloscope BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING ELECTROMECHANICAL FEATURED FILTER DESIGN HARDWARE JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER VALVE COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF