KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AKIPONGEZA KIWANDA CHA VIATU GEREZA KARANGA MJINI MOSHI - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 18 February 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AKIPONGEZA KIWANDA CHA VIATU GEREZA KARANGA MJINI MOSHI

kil1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kil2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.
kil3
Fundi wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda hicho.
kil4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.
kil5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Maafisa wa Magereza, Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mara baada ya kumaliza kukitembelea Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Rwegasira alikipongeza kiwanda hicho na kulitaka Jeshi la Magereza kuongeza juhudi zaidi katika uzalishaji wa viatu.
kil6
Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Anderson James akimpa zawadi ya viatu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kukikagua kiwanda hicho pamoja na kujifunza jinsi ya utengenezaji wa viatu unavyofanyika. Kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment