'IWAPO WANAWAKE WATAJUA HAKI ZAO, WATAENDELEA' - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Saturday, 6 February 2016

'IWAPO WANAWAKE WATAJUA HAKI ZAO, WATAENDELEA'

'Iwapo wanawake watajua haki zao, wataendelea'
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za wanawake amezungumzia umuhimu wa kila mwanamke kufahamu haki zake na kuongeza kuwa, ikiwa wanawake watafanikiwa katika uga huo, basi wataweza kutetea haki zao hata katika asasi za kimataifa.
Elham Aminzadeh, ameyasema hayo katika mahfali ya kufungu kozi za kuinua ujuzi wa wanawake katika ngazi ya kimataifa na kuongeza kuwa, kozi hizo ni muhimu sana kwa ajili ya sekta binafsi, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Elham Aminzadeh amesema kwamba, ikiwa wanawake watakuwa na welewa sahihi na wa kutosha katika masuala ya sheria, bila ya shaka wataweza kwa vipindi tofauti kusimama imara katika ngazi ya kimataifa na kujibu hoja kwa uhakika.
Amesema ni jambo la dharura kwa wanawake kuwa na welewa wa kutosha kuhusu sheria za kimataifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za wanawake ameongeza kuwa, ni jambo lililo bora kuzingatiwa utekelezaji wa sheria na mikataba inayohusiana na wanawake katika nchi nyingine za dunia. Aidha amesema kuwa, hii haina maana kwamba, mfumo wa nchi yoyote ya Ulaya unaweza kuwa sahihi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Post a Comment