BODI TSN YAMSIMAMISHA KAZI MHARIRI MTENDAJI - LEKULE

Breaking

23 Feb 2016

BODI TSN YAMSIMAMISHA KAZI MHARIRI MTENDAJI

DI1
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba(wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki (hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi hiyo  Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi(Picha na Daudi Manongi)
DI2
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye akiongea na vyombo vya Habari kuhusu maagizo aliyoyatoa kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya serikali TSN ikiwemo sababu za wafanyakazi wengi kuacha kazi katika shirika hilo.
DI3
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitembezwa kuonyeswa mazingira ya kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni mhariri mtendaji wa kampuni hiyo ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki ambaye amesimamishwa kazi kutokana na utendaji usiorizisha  na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba.
DI4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mchapaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN) Bw.Paul Kasele alipofanya ziara katika shirika hilo jana jijini Dar es Salaam.

DI5
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN jana jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo  Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana  na utendaji usioridhisha  ndani ya kampuni hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.
“Kumekuwa  na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa  majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.
Aidha Prof Warioba  ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.
Hatua hiyo  ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika  Kampuni hiyo  ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea    wafanyakazi 21  kuacha kazi.
“Nataka Bodi itafakari juu ya  malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.
Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni  ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa

No comments: