ASKARI WALIOFARIKI KATIKA MSAFARA WA RAIS MAGUFULI WAAGWA SINGIDA - LEKULE

Breaking

8 Feb 2016

ASKARI WALIOFARIKI KATIKA MSAFARA WA RAIS MAGUFULI WAAGWA SINGIDA

IMG_3064
Askari watatu wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, waliofariki dunia wakiwa kwenye msafara wa rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya gari lao walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na dereva kushindwa kulimudu wakitokea Singida kuelekea Dodoma wameagwa jana. Zifuatazo ni picha za tukio hilo la kuaga miili ya askari hao.
IMG_3093
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, akitoa salamu za pole kutoka kwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini, Ernest Mangu na polisi mkoa wa Singida kwa familia za askari polisi watatu waliofariki dunia wakati wakiwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli jana kutoka Singida Dodoma.
IMG_3111
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Manyara, ACP Camilius Wambura, akitoa salamu za pole kwa familia na jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na askari polisi watatu waliokuwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli wakitokea Singida kuelekea Dodoma juzi.
IMG_3113
Mkuu wa mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone, akitoa salamu za pole kwa familia na jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na askari 3 kwenye ajali iliyotokea Isuna kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli uliokuwa ukitokea Singida kuelekea Dodoma juzi.
IMG_3049
Askari polisi mkoa wa Singida,wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Insp.Miraji mwigelo Kindamba,Insp.Kindamba ni moja kati ya askari 3 waliofariki juzi kwenye ajali iliyotokewa kwenye msafara wa Dk. Magufuli uliokuwa ukitokea Singida kwenda Dodoma.
IMG_3078
Baadhi ya mamia ya waombolezaji wa msiba mkubwa wa askari polisi watatu waliofariki juzi wakiongoza msafara wa rais Dk.Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma.(Picha zote na Nathaniel Limu).

No comments: