Zidane aanza na ushindi, Bale apiga hat trick - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 10 January 2016

Zidane aanza na ushindi, Bale apiga hat trick

3873

Kocha mpya wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameanza vyema kazi ya kuiongoza klabu hiyo kwa kupata ushindi wa goli 5 kwa bila dhidi ya Deportivo La Coruna katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania uliochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Magoli ya Real Madrid katika mchezo huo yalifungwa na Karim Benzema dk. 15 na 90 na Gareth Bale (pichani) aliyefunga hat trick dk. 23, 49 na 63.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Zidane alisema mchezo huo umekuwa mzuri kwake na kila jambo ambalo alikuwa amelipanga limetokea kama jinsi alivyokuwa akitarajia na amependezwa na hali ya mchezo ilivyokuwa.
“Nimependa hali ya mchezo kwa ujumla, tumeshinda goli 5 haikuwa rahisi kwa timu kama La Coruna nina furaha sana na mchezo, nimependa hali ya mchezo, kwa waliocheza na ambao hawakucheza,” alisema Zidane.

Aliongeza kuwa baada ya matokeo hayo mazuri kutawapa nafasi ya kufanya mazoezi zaidi ili wazidi kuwa bora kwa michezo iliyopo mbele yao na anaamini watafanikiwa kwa michezo mingine inayowakabili.
Post a Comment