Mkurugenzi
wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya
Idarous Khamsin (katikati) akimtambulisha rasmi mwanadada, Wema Sepetu
(kushoto) ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. (Kulia) ni Martin Kadinda
ambaye naye miongoni mwa watendaji wanaoratibu jukwaa hilo la Lady in
Red. katika usiku wa Lady In Red fashion show 2016, litakalofanyika 31
Januari ndani ya ukumbi wa Danken House wa Mikocheni jijini Dar es
Salaam.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Nyota
wa filamu za Bongo, ambaye pia aliwai kuwa Miss Tanzania kipindi cha
nyuma, Wema Issac Sepetu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye onesho na
jukwaa maalum la mitindo la kila mwaka la “Lady In Red 2016”
litakalofanyika 31 Januari katika ukumbi wa Danken House uliopo
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya
Idarous Khamsin amebainisha hilo alipokutana na badhi ya wabunifu wa
mavazi na wanamitindo watakaopamba jukwaa hilo hiyo 31 Januari, ambapo
amewataka kujipanga ilikuchangamkia fursa ya kupata kuinua tasnia ya
mitindo nchini.
“Lady
In Red fashion show 2016 ni ya kipekee na jukwaa hili ni fursa kwa
kuinua wabunifu wa mavazi chipukizi kupata kuonekana zaidi na hata
kukuza majina na ubunifu wao kujulikana ndani na nje” amefafanua Mama wa
Mitindo, Asya Idarous.
Aidha,
ameeleza kuwa, ilikutoa msisimko zaidi kwa jukwaa hilo. Mwanadada Wema
Sepetu ndiye atakaye bariki siku hiyo ikiwemo utoaji wa vyeti kwa
washiriki ilikuweka kumbukumbu.
Asya
Idarous ameongeza kuwa, hadi sasa jukwaa hilo la Lady in red linafikia
umri wa miaka 12 litaendelea kuwa juu zaidi na kuwa shule kwa tasnia ya
mitindo ambapo kwa sasa pia linafanyika na nje ya Tanzania ikiwemo
nchini Uingereza.
Hata hivyo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliunga mkono ikiwemo kudhamini onesho hilo.
Mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady Inn Red fashion show 2016 kama inavyoonekana pichani.
Mwanadada
Wema Sepetu akitoa nasaha zake kwa Wabunifu wa mavazi na wanamitindo
(hawapo pichani) wakati wa utamburisho wa jukwaa la Lady In Red fashion
show 2016 linalotarajiwa kufanyika 31 Januari.
Martin
Kadinda akitoa nasaha zake kwa wabunifu na wanamitindo waliojitokeza
katika mkutano huo (hawapo pichani) kuhusiana na jukwaa la Lady In Red
fashion show 2016.
No comments:
Post a Comment