Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Gari aina ya Noah Kugongana Uso kwa Uso na Basi la Adventure Mkoani Dodoma - LEKULE

Breaking

25 Jan 2016

Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Gari aina ya Noah Kugongana Uso kwa Uso na Basi la Adventure Mkoani Dodoma


Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya toyota Noah yenye namba za usajili T243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso kwa uso na basi la abiria la kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam katika kijiji cha Buingiri madukani wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
 
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 9 alasiri ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na abiria waliokuwa ndani ya basi walisema ajali hiyo imetokana na mwendokasi wa gari aina ya Noah ambalo dereva wake alipoteza mwelekeo na kisha gari hilo kuhama na kulivaa basi na watu watatu kupoteza maisha papo hapo huku mmoja akijeruhiwa vibara.

Muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Dodoma lilifika eneo hilo na kukuta msongamano mkubwa wa magari kutokana na ajali hiyo kuziba eneo la barabara hali iliyowalazimu kuyaondoa magari hayo ili kuruhusu shughuli zingine kuendelea.

kwa upande wake kamanda wa polsi mkoa wa Dodoma David Misime akizungumza katika eneo la tukuio aliwataja miongoni mwa watu waliofariki dunia ni dereva wa Noah aliyetambulika kwa jina la Abdalah Said Hajiru mkazi wa Dar es Salaam huku maiti nyingine mbili zikishindwa kutambulika mara moja ambapo pia jeshi hilo lilifanya jitihada za kuwatafutia basi lingine abiria ili waendelee na safari yao.

Awali kabla ya vikosi vya usalama kufika eneo hilo wananchi wenye hasira walifunga barabara kwa magogo wakidai kuwa wamechoshwa na ajali katika eneo hilo na kuitaka serikali kupitia wakala wa barabara nchini Tanroads kuweka matuta ili kupunguza ajali.

No comments: