Wahariri wa Mawio, MwanaHALISI waachiwa kwa dhamana - LEKULE

Breaking

20 Jan 2016

Wahariri wa Mawio, MwanaHALISI waachiwa kwa dhamana


MHARIRI wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI ambaye pia ni mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa jana wameachia kwa dhamana na Jeshi la Polisi, baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo.

Wahariri hao walijisalimisha juzi  majira ya saa tisa jioni baada ya kupokea taarifa ya kutafutwa na jeshi la polisi kwa siku tatu na kuhojiwa kwa masaa nane, lakini walipomaliza majira ya saa tano usiku walinyimwa dhamana na polisi kwa madai jana asubuhi wangepelekwa mahakamani.

Jeshi la polisi walishindwa kuwapeleka mahakamani wahariri hao, lakini walifungua dhamana kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwekewa dhamana ya Sh. 20 milioni, huku akitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili.

Mkina na Jabir wametimiza masharti hayo kwa kudhaminiwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja huku kila mdhamini akisaidi bondi ya Sh. 10 milioni.


Wahariri hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa mbili asubuhi mpaka hapo watakapopewa utaratibu mwingine.

No comments: