WAFANYAKAZI 350 WA KIWANDA CHA SUKARI CHA MAHONDA WAKOHATARINI KUPOTEZA AJIRA ZAO.

 Baadhi ya Miwa iliyoteketea kwa moto kutokana na hujuma iliyofanywa na Watu wasiojuilikana huko kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa Pole Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta kufuatia watu wasiojuilikana kutia tena moto mashamba ya Miwa Mahonda.
  Balozi Seif kati kati akifuatana na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda akikagua baadhi ya sehemu ya shamba la Miwa la Eka 50 lililotiwa moto jana jioni na watu wasiojuilikana.
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa.
 Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara iliyopatikana kutokana na hujuma ya moto kwenye mashamba ya Miwa Mahonda.
Balozi Seif akielezea masikitiko yake kutokana na baadhi ya watu kufanya hujuma za makusudi kujaribu kuvuruga juhudi za Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda za kuimarisha Sekta ya Viwanda.


TISHIO la ajira za Wafanyakazi 350 wa Kiwanda cha Sukari Mahonda zinaendelea kuwa hatarini kufuatia hujuma zinazofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu kuendelea kutia moto mashamba ya miwa huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kitendo hicho cha hujuma kinaweza kuusababisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kuwa na mawazo ya kufikiria kuzuia ajira mpya 450 za Wafanyakazi wa Kiwanda hicho katika malengo yake baada ya kukamilika kwa matengenezo makubwa na kuanza tena uzalishaji wa sukari.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta alisema hayo wakati akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kuangalia hasara iliyosababishwa na moto uliotiwa kwa mara nyengine tena na Watu wasiojuilikana ndani ya shamba la Miwa katika kipindi cha siku Tano baada ya tukio kama hilo la Tarehe 30 mwezi uliopita.
Bwana Tushar alisema moto huo umetiwa kati kati ya shamba la Miwa jana jioni na wahalifu wenye dhamira ya makusudi ya kutoa usumbufu na kizuizi kwa wananchi na vikosi vya Ulinzi katika harakati za kukabiliana na moto huo. .
Alisema Eka zipatazo 50 za Miwa iliyopevuka imeteketea kwa moto hali ambayo imeisababishia Kiwanda hicho hasara ya Tani 200 za Sukari na Lita 2,300 za Spititi zilizokuwa zizalishwe kutokana na miwa hiyo ikiwa na hasara ya jumla ya dola za Kimarekani Laki 228,758.56 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 494 za Kitanzania.
Meneja huyo wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda alifahamisha kwamba hadi sasa Eka zipatazo 200 zimeteketea kwa moto kwenye matukio yote mawili katika kipindi cha siku Tano zilizopita na kusababisha hasara ya jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 1,176,234.28 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 2,326,818,500/-.
Akiupa pole Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kutokana na hasara ya Mashamba iliyosababishwa na moto huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hujuma hiyo ya makusudi haiitakii neema Zanzibar katika harakati zake za kustawisha uchumi wake.
Balozi Seif aliwanasihi watu wenye tabia hiyo kuachana nayo kwani mbali ya kujibebesha dhambi lakini pia inawavunja moyo wawekezaji walioamua kuja kuwekeza miradi yao ya kiuchumi Nchini kwa lengo la kuisaidia Serikali pamoja na Wananachi hapa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba juhudi za makusudi za Serikali kuu katika kukifufua tena Kiwanda cha Sukari na Manukato Mahonda baada ya kusita kwa miaka kadhaa zililenga kuimarisha  Uchumi kupitia sekta ya viwanda sambamba na kupanua soko la ajira kwa Vijana.
Alisema tabia ya baadhi ya watu kufikiria kwamba hujuma hiyo itatoa fursa kwao kutumia maeneo ya mashamba ya Miwa kuendeleza Kilimo na Mifugo inafaa kuachwa mara moja kwa vile mashamba hayo yataendelea kuwa katika mipango ya Serikali ya kuhudumia Sekta ya Viwanda.
“ Haya ni Mashamba ya Serikali yaliyotengwa maalum kwa shughuli za harakati za Viwanda. Hivyo ndoto za baadhi ya Watu kufikiria kwamba hujuma zao zitazaa matunda kwa kufanya wanavyotaka zinapaswa ziachwe mara moja ”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliufahaisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kwamba Serikali Kuu inaangalia mpango utakaowezesha Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia ulinzi kwenye Mashamba hayo ili kulinda hujuma zinazoonekana kushamiri siku hadi siku.
Hilo ni tukio la sita la hujuma za moto kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda tokea kianze tena uzalishaji wa sukari na Spiriti mapema mwaka uliopita wa 2015.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/1/2016.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF