UN: Maelfu ya raia wameuawa Iraq - LEKULE

Breaking

20 Jan 2016

UN: Maelfu ya raia wameuawa Iraq

Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq
Umoja wa Mataifa unasema kuwa ghasia zinazowakumba raia nchini Iraq ni nyingi huku takriban watu 18,800 wakiuawa kati ya tarehe mosi mwezi Januari mwaka 2014 na 31 mwezi Oktoba mwaka 2015.
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi katika kipindi hicho kulingana na ripoti mpya ya UN.
Umoja wa mataifa unawalaumu wanamgambo wa Islamic State kwa kuendesha ghasia na kuwashikilia watumwa watu 3,500, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
Islamic state wanawashikilia watumwa 3,500 wengi wakiwa ni wanawake na watoto
Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Zeid Raad Al Hussein anasema ripoti hiyo inaonyesha kile wakimbizi kutoka Iraq wanatoroka wakati wanakimbilia Ulaya na maeneo mengine.
Ripoti hiyo inatokana na mahojiano na wale waliohama makwao na ushuhuda wa moja kwa moja kutoka kwa waathiriwa au wale walioshuhudia ukiukaji wa haki za binadamu
Ripoti hiyo inasema kuwa idadi ya raia waliouawa kati ya tarehe 1 Januari mwaka 2014 na Oktoba 31 mwaka 2015 ni 18,802 na waliojeruhiwa 36,245.

Umoja huo hata hivyo unatahadharisha kwamba idadi halisi huenda ikawa juu zaidi.

No comments: