UKAWA Washinda Kiti ca Umeya Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam - LEKULE

Breaking

16 Jan 2016

UKAWA Washinda Kiti ca Umeya Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (katikati) akiongoza sala ya kufungua mkutano wa kwanza baada ya uchaguzi wa kumchagua Meya na Naibu Meya wa manispaa hiyo.
******

Hatimaye baada ya danadana za muda mrefu, uchaguzi wa kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja wa Vyama vinavyunda Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanikiwa kuongoza Manispaa hizo.

Chaguzi hizo zilizhairishwa mara mbili kutokana na mvutano uliotokewa katika chaguzi za nyuma, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa amri za mahakama.

Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa hiyo baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepata kura 20. Naibu Meya ni Diwani wa Tandale kwa tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.

Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala  leo pia uliingia katika mgogoro kati ya madiwani wa CCM na wale wa Ukawa, hali iliyosababisha CCM kususia uchaguzi huo na kuwaacha Ukawa kupiga kura peke yao na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kumtangaza Charles Kuyeko (Chadema) kuwa mshindi wa kiti cha Meya wa Ilala kwa ushindi wa  kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) ambaye amepata kura 31.

Jumla ya madiwani waliotakiwa kupiga kura katika uchaguzi huo ni 54, hivyo madiwani 31 wa Ukawa waliobaki ndani walitimiza akidi ya uchaguzi huo kuendelea.


Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi  wa kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya,naibu Maya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakishangilia ushindi wa Maya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.
 Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi wakiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee. 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na kuwashukuru madiwani leo jijinin Dar es Salaam.

No comments: