TRL Yasitisha Kwa Muda Safari Za Treni Ya Bara Kutokana Na Mafuriko Kati Ya Morogoro Na Dodoma - LEKULE

Breaking

3 Jan 2016

TRL Yasitisha Kwa Muda Safari Za Treni Ya Bara Kutokana Na Mafuriko Kati Ya Morogoro Na Dodoma

KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia  Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko.

Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.

Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119. wa treni hiyo.

Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia  Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala. 

Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena.

Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya  

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar es Salaam,
Januari 02, 2016

No comments: