Tazama Video hii Na Maelezo Ya Mh Mwigulu Nchemba Akitumbua Vijipu Uchungu huko TUNDURU, RUVUMA. - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Saturday, 16 January 2016

Tazama Video hii Na Maelezo Ya Mh Mwigulu Nchemba Akitumbua Vijipu Uchungu huko TUNDURU, RUVUMA.


Ufuatiliaji wa Ugawaji wa pembejeo kwa wakulima,Nimefika wilaya ya Tunduru,Kata ya Nandembo na kata jirani kwaajili ya kujiridhisha na namna ugawaji wa pembejeo unavyofanyika kwa wakulima.
 
Nimekutana na mchezo mchafu wa ugawaji wa pembejeo unaohusisha wakala wa pembejeo kula njama na viongozi wa serikali wa kata na vijiji kuwasainisha wakulima kuwa wamepokea pembejeo(Mbegu +Mbolea) ilia hali pembejeo hizo zinaishia mifukoni mwa wakala.
Baadhi ya wakulima ambao sio waaminifu wanadiriki kupokea fedha kidogo iliwamuachie wakala zile pembejo akauze sehemu nyingine kwa bei ya juu ili hali ni ruzuku iliyotolewa na serikali kwaajili ya kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo chao.
 
Kwa hatua za awali kwa ubadhilifu uliofanywa na Uongozi wa kata ya Nandembo na mawakala waliopewa dhamana kusambaza pembejeo hizo wote wamekamatwa na jumatatu kupitia Kamati ya Ulinzi ya wilaya watapandishwa kizimbani.
Lakini kuanzia sasa wakala Bw.Zuberi Namahala na Bw.Ibrahim Mohamed Ibrahim mbali ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani,kuanzia sasa wamefutwa kwenye orodha ya mawakala wa pembejo.

Natoa rai kwa Viongozi,Mawakala wa pembejeo na wakulima wote popote walipo kuhakikisha lengo la serikali la kuinua sekta ya Kilimo inafanyika kwa uaminifu na ufanisi,kwa yeyote yule anayeshiriki kuhujumu na kujinufaisha kupitia pembejeo zinazotolewa na serikali hatakwepa mkono wa serikali.
Imetolewa na Mwigulu L. Nchemba,
Waziri wa Kilimo,ufugaji na uvuvi.
==>Tazama video hii Waziri wa kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Mh Mwigulu Nchemba akitumbua vijipu uchungu huko TUNDURU, RUVUMA....


Post a Comment