Naibu Katibu Mkuu (Tamisemi) Dk. Deodatus Mtasiwa akitoa ufafanuzi wa jambo kwenye mkutano huo na wanahabari (hawapo pichani).
Kutoka
kushoto ni, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk. Neema
Rusibamayila, Naibu Katibu Mkuu (Tamisemi), Dk. Deodatus Mtasiwa na
Kaimu Katibu Mkuu, John Michael.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na
Watoto leo imetoa ripoti yake ya wiki juu ya mwenendo wa kipindupindu
hapa nchini.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za wazara hiyo,
Mkurugenzi wa Huduna za Kinga Nchini, Dk. Neema Rusibamayila amesema
kuwa katika kipindi cha wiki moja kuanzia Januari 11 hadi 17,2016
kulikuwa na wagonjwa wapya 549 na vifo 10 huku mikoa iliyoripoti kuwa na
ugonjwa ikiongezeka kutoka 11 hadi kufikia 16 ukilinganisha na wiki
iliyopita.
Rusibamayila
amesema, mikoa hiyo iliyoongezeka kwa kurudia kuripoti wagonjwa wapya
baada ya kudhibiti ugonjwa kwa wiki zilizopita ni Dar es Salaam, Lindi,
Rukwa, Kagera na Kilimanjaro huku akiongeza kuwa bado kuna mikoa
inaendelea kuripoti wagonjwa ikiwa ni pamoja na Morogoro, Arusha,
Singida, Manyara, Pwani ,Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu.
Aidha,
alisema Mkoa wa Morogoro unaendelea kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa
(Manispaa ya Morogoro wagonjwa 120, Halmashauri ya Morogoro wagonjwa 40 )
ikifuatiwa na Mkoa wa Simiyu wenye idadi ya watu 50.
Hata
hivyo, Rusibamayila ameeleza namna mwananchi anavyoweza kupata huduma ya
kufahamu dalili za ugonjwa huo wa kipindupindu kupitia njia ya simu ya
mkononi kwa kupiga namba 117 kisha kusikiliza ujumbe wa sauti, au
kuandika ujumbe wa maneno “kipindupindu/cholera” kwenda namba 15774 na
huduma hiyo haina malipo yoyote kwa mtumiaji.
Alisema
kuanzia Agosti mwaka jana ugonjwa huo ulipoanza hapa nchini hadi jana
Januari 17, 2016 jumla ya watu 14,105 wameugua ugomjwa huo na kati yao
218 wamepoteza maisha kwa maradhi hayo ya kipindupindu.
No comments:
Post a Comment