Serikali Yaahidi Kuendelea Kushusha Kodi kwa Wafanyakazi - LEKULE

Breaking

28 Jan 2016

Serikali Yaahidi Kuendelea Kushusha Kodi kwa Wafanyakazi



Serikali imesema imeadhimia mwaka wa fedha wa 2016/2017 kushusha kiwango cha tozo la kodi kwa mfanyakazi kutoka asilimia 11 ya hivi sasa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka huo wa fedha.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo bungeni ambapo amesema kuwa lengo la serikali ni kushusha zaidi hadi kufikia digiti moja.

Waziri Kijaji ameongeza kuwa baada ya kufikia asilimia 10 ya tozo la kodi hiyo serikali itakaa na wadau ikiwemo vyama vya wafanyakazi ili kutafuta ufumbuzi wa ni namna gani wanaweza kushusha zaidi kutokana na ukuaji wa uchumi siku hadi siku.

Katika hatua nyingine waziri Kijaji amesema kuwa serikali imedhamiria kupandisha kiwango cha pensheni kwa wazee wastaafu hadi kufikia shilingi laki mbili na nusu kadri ya uchumi utakavyoimarika na mikakati tayari imeshaanza kuandaliwa.

No comments: