RAIS MAGUFULI NDANI YA COMBAT ALISISIMUA JIJI LA ARUSHA KWA MAVAZI YA KIJESHI NA HOTUBA

 
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo asubuhi.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
 Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo ya zana mojawapo ya zana za Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha. Picha na IKULU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

 

Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameonya kuwa wilaya ama Mkoa wowote ambao utakumbwa na njaa, itakua ni kipimo tosha cha kuonesha kuwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa wilaya husika hafai kuendelea na wadhifa huo.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti aliposimamishwa na wananchi wa Arusha Mjini akiwa njiani kuelekea Monduli ambako amefunga  "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililoandaliwa na kutekelezwa na kamandi ya Jeshi la nchi kavu ambalo ni sehemu ya jeshi la wananchi wa Tanzania.

Amesema kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, Viongozi wa Wilaya na Mikoa wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi kuzalisha mazao ya chakula ili wasikumbwe na njaa.

Rais Magufuli ameendelea kuwasihi wananchi wa Arusha Mjini kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba kilichobaki sasa ni kazi huku akiwahimiza kufanya kazi za uzalishaji mali ikiwemo kilimo.

"Naomba ndugu zangu mniombee, na ninapenda kuwahakikishia kuwa sitawaangusha. Yote niliyoahidi nitayatekeleza bila kubagua nawaombeni mnipe muda na muwe wavumilivu" alisisitiza Rais Magufuli.

Amerejea kauli zake alizozitoa jana alipoingia mkoani Arusha kuwa atendelea kuwashughulikia wezi, mafisadi na watendaji wote wa serikali ambao wamekua wakijineemesha kwa kufuja mali ya umma kupitia kampeni yake ya "Kutumbua Majipu" na amewaomba watanzania wote waendelee kumuombea ili atumbue majipu yote hadi yaishe.

 Rais Magufuli amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini waliokuwa wamekusanyika kwa maelfu kando kando mwa barabara na hivyo kujikuta akisimamishwa na wananchi wa Sanawali, Tekniko, Ngarenaro, Kona Ya Nairobi, Mbauda, Majengo Na Kisongo.

Akiwa katika eneo la Ngarenaro wananchi wamelalamikia vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso na pia katika eneo la Kona ya Nairobi wananchi wamelalamikia kero za kelele na uchafu wa kiwanda kilichojengwa kandokando mwa barabara ambapo Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi kero hizo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.
22 Januari, 2016
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF