Hello

Welcome lekule blog

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation.
together in the world. #lekule86
Join us on

Raia wa Kigeni 15 katika mgodi wa Tanzanite One wafukuzwa nchini.

Kaimu Katibu Mkuu mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto (aliyesimama) akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha ambazo zinashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini katika kudhibiti utoroshaji madini ya Tanzanite nje ya nchi. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hizo, Amos Makala. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kulia)na wa Tatu kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje.
Mwenyekiti wa Kikosi kazi kinachoshughulikia udhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi, Muliro Muliro (aliyesimama) ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, akitoa taarifa ya Kikosi Kazi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Amos Makala (wa kwanza kulia) wakati wa kikao cha Kamati hizo kilichofanyika jijini Arusha.Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kulia) na wa Tatu kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha wakiwa katika kikao cha Kamati hizo kilichofanyika katika kituo cha Jimolojia mkoani Arusha. Kamati hizo zinashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi na ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni zinazoshughulika na biashara ya madini nchini.
Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara katika Wizara ya Nishati na Madini, Salim Salim (aliyesimama) akitoa taarifa ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na Wizara ya Nishati na Madini katika ya udhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi na ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni zinazoshughulika na biashara ya madini nchini wakati wa kikao cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha kilichofanyika katika Kituo cha Jimolojia jijini Arusha. Wa Tano kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hizo, Amos Makala na wa nne kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe.

Teresia Mhagama na Mohamed Saif

Jumla ya raia wa kigeni 15 waliobanika kufanya kazi kinyume na taratibu za kisheria  katika mgodi wa Tanzanite One uliopo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wameondoshwa nchini tarehe 25 Desemba, mwaka jana.

Hayo yalielezwa jana jijini Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Amos Makala wakati wa kikao chake na wajumbe wa kamati  hizo pamoja na Naibu Katika Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe kilichofanyika katika Kituo cha  Jimolojia jijini humo.

Alisema kuwa raia hao waliamuliwa kuondoka nchini na Idara ya Uhamiaji mkoani Manyara ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa hiyo ambazo ziliunda kikosi kazi cha wajumbe 13 kwa ajili ya udhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi, ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni zinazoshughulika na biashara ya madini na kuchunguza raia wa kigeni wasiokuwa na sifa za kufanya kazi kwenye migodi pamoja na kampuni za madini. 

 “Amri hiyo ya kuondoka nchini ndani ya siku saba ilianza kutekelezwa kuanzia tarehe 17 Desemba, 2015 na raia wote hao waliofukuzwa  wanatoka nchini India. Nakipongeza Kikosi kazi hiki ambacho kimeanza kutekeleza majukumu ya kamati kwa ufanisi na zoezi hili litakuwa ni endelevu,” alisema Makala. 

Aidha, alisema kuwa kikosi kazi hicho kilifanya operesheni ya siku mbili katika Mikoa hiyo kwa lengo la kukamata wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite ambao hawana leseni ambapo  jumla ya wafanyabiashara 15 walikamatwa mkoani Arusha wakati mkoani Manyara idadi ya wafanyabiashara waliokamatwa kwa tuhuma za aina hiyo ni Nane na madini waliyokamatwa nayo yana thamani ya takribani shilingi milioni 47.  

Alisema kuwa operesheni hiyo iliyofanyika tarehe 30 na 31 mwezi Desemba mwaka jana ilijikita pia katika kuwabaini raia wa kigeni wanaofanya biashara ya madini bila vibali ambapo raia mmoja kutoka nchini Ethiopia alikamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara ya madini kinyume na sheria na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za awali za kipelelezi kukamilika.

Awali, Mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho, Muliro Muliro ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha alisema kuwa baada ya zoezi la kuwabaini pamoja na kuwakamata wafanyabiashara wa madini wasiokuwa na vibali, jumla ya wafanyabiashara 272 ambao walikuwa wakifanya biashara hiyo kinyemela walijitokeza katika Ofisi za Madini za Arusha na Merelani ili kuomba leseni za kufanya biashara hiyo.

“Mkoani Manyara (Merelani) ilipo migodi ya Tanzanite jumla ya wafanyabiashara 154 walijitokeza na kuwasilisha maombi ya leseni za wakala wa madini ya vito (brokers’ licence) na hivyo hadi kufikia tarehe 8 Januari mwaka huu, kiasi cha shilingi milioni 38.5 zilikusanywa kutokana na ada ya maombi ya leseni husika,” alisema Muliro.

Vilevile alisema kuwa kwa upande wa Arusha, maombi mapya ya leseni za wakala wa madini yapatayo 115 yaliwasilishwa Ofisi za Madini za kanda ya Kaskazini na hivyo kiasi cha shilingi milioni 28.7 kimekusanywa kutokana na maombi hayo.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Profesa Mdoe alizipongeza Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi, kubaini wafanyabiashara wa madini hayo wasiokuwa na vibali na wanaokwepa kulipa kodi stahiki.

Alisema kuwa bado kuna kazi kubwa mbele ya kuhakikisha kuwa suala hilo linakomeshwa na kusisitiza kwamba kila mtumishi anapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo huku akieleza kuwa operesheni haitoweza kumaliza tatizo hilo kama watumishi hawatatimiza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi ili kutotoa mianya kwa matatizo hayo kuendelea kuwepo.

Share this:

ABOUTME

Hi all. This is deepak from Bthemez. We're providing content for Bold site and we’ve been in internet, social media and affiliate for too long time and its my profession. We are web designer & developer living India! What can I say, we are the best..

Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Labels

LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC ROBOTICS DIGITAL SEMICONDUCTORS GENERATOR AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING REFERENCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT TRANSDUCER & SENSOR VIDEO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE TEARDOWN SYNCHRONOUS GENERATOR DIGITAL ELECTRONICS ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES AUTOMOTIVE MICROCONTROLLER SOLAR PROTECTION DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES WEARABLES CAMERA TECHNOLOGY COMMUNICATION GENERATION BATTERIES FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE CONTROL SYSTEM NUCLEAR ENERGY SMATRPHONE FILTER`S POWER BIOGAS BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS ENERGY SOURCE PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD BLUETOOTH C PROGRAMMING HOME AUTOMATION HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY COMPUTER DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS USB ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS CONTROL MOTION ELECTRICAL LAWS INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES APPS & SOFTWARE BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RECTIFIER AND CONVERTERS RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS DC MOTOR DRIVES ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS WIRELESS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION INDUSTRIAL DRIVES LAPTOP SCIENCE THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART oscilloscope BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING ELECTROMECHANICAL FEATURED FILTER DESIGN HARDWARE JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER VALVE COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF