NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 1 January 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHININaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Dkt. Kolimba kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait. 
Mhe. Balozi Al Najib akimkabidhi Mhe. Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.
Mhe. Dkt. Kolimba nae akimshukuru Balozi Al Najib kwa kuwasilisha salamu hizo za pongezi na kwamba amezipokea na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kuwait katika masuala mbalimbali ya maendeleo. 
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Kolimba na Balozi wa Kuwait hapa nchini (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Batholomeo Jungu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Tahir Bakari, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri. 

Picha ya pamoja.
Post a Comment