Mwanamuziki Mos Def afurushwa A Kusini - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 17 January 2016

Mwanamuziki Mos Def afurushwa A Kusini

Mos Def
Mwanamuziki wa muziki wa Rap kutoka Marekani kwa jina maarufu Mos Def ameamrishwa kuondoka Afrika Kusini katika kipindi cha siku 14 baada ya kukamatwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji.
Mos Def anayejulikana kama Yasiin Bey alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cape Town siku ya Alhamisi baada ya kujaribu kuondoka nchini humo na stakhabadhi bandia.
Idara ya maswala ya ndani imesema kuwa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42 alitoa kile alichokitaja kuwa pasipoti ya dunia.
Imesema kuwa mwanamuziki huyo alikaa sana nchini humo kinyume na visa yake ya utalii aliyopata mwaka 2013.
Akiwa amezaliwa na kuitwa jina Dante Smith mjini New york,bwana Bey kwa sasa amepigwa marufuku nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka mitano,lakini amepewa haki ya kukata rufaa.
Cape Town
Amekuwa akiishi mjini Cape Town tangu mwezi May mwaka 2013 kulingana na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.
Akiwa ameteuliwa kuwania tuzo sita za Grammy,ameshiriki katika filamu kadhaa,ikiwemo The HitchHikers Guide to Galaxy,Be Kind Rewind na Italian Job.
Post a Comment