MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, "WATOA SOMO KWA WAHARIRI JUU YA KAZI NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA MFUKO - LEKULE

Breaking

30 Jan 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, "WATOA SOMO KWA WAHARIRI JUU YA KAZI NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA MFUKO

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba akitoa mada kwa Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania chini ya Jukwaa la Wahariri, (TEF) wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TEF mjini Morogoro leo Januari 29.01.2016. Mshomba aliwaeleza Wahariri hao WCF  inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka huu wa 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008. (Picha na Imma Matukio)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba kutoa mada katika ukumbi wa Nashera Morogoro. WCF inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008
 Mhariri Haura Shamte akizungumza
 Mhariri Balinagwe Mwambugu, akizungumza
 Mhariri Paul Maregesi, akizungumza
 Picha ya pamoja
Bw. Msomba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mada yake

No comments: