DSC_5186
Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) (katikati) akiwa pamoja na wanasheria wanaosimamia kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa kwa wakazi wa mabondeni waliopo kweny mabonde ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Awali 14 Januari mwaka huu  Mahakama Kuu ya Ardhi  ilisogeza mbele usikilizwaji wa kesi ya msingi ya  kupinga kubomolewa kwa nyumba za Mabondeni hasa zile zilizopo kwenye bonde la jimbo hilo la Kinondoni. 

Hata hivyo inaelezwa kuwa leo inaweza hali ikawa tofauti kwa wananchi wa mabondeni wanaofika kusikilizwa kesi yao kwani jibu lolote litakalotoka litakuwa mwiba kwao na kufanya hali kuwa ngumu kwa upande huo wa wananchi ambao jicho na sikio lao wakilielekeza kwa Mbunge wao pamoja na Mawakili wanaosikiliza kesi.
“Wanasema mbichi mbivu basi kujulikana mchana wa leo 25 Januari. Maamuzi ya Mahakama Kuu ya Ardhi itakayoyatoa ndio mwisho wa utata na hali halisi ya tukio linaloendelea sasa” kilieleza chanzo kutoka kwa watu waliokwenye kamati ya kushughulikia kesi hiyo wanaoishi mabondeni.
Hata hivyo mbichi na mbivu ni  kwa wakazi hao wa mabondeni ambao licha ya waliobomolewa, pia wapo ambao  nyumba zao zimewekewa alama ya X wakitakiwa kuzibomoa maramoja huku wengine wakiwa na wasiwasi ya kubomolewa baada a kutoelewa kama wapo bondeni ama sehemu ambayo hairuhusiwi kwa shughuli za makazi.