MAN UTD YAKWAMA TENA OLD TRAFFORD - LEKULE

Breaking

24 Jan 2016

MAN UTD YAKWAMA TENA OLD TRAFFORD


United vs South 2
United vs South 2Klabu ya Manchester United imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kujikuta ikigaragazwa kwa bao 1-0 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
United vs South 3
United vs South 3
Ilimchukua dakika saba na sekunde 43 tu, Charlie Austin kuiandikia bao Southampton akitokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mane. Austin aliweka mpira wavuni dakika ya 87 akiunganisha kwa kichwa krosi ya James Ward-Prowse na kuipa ushindi timu yake ikiwa kwenye uwanja wa ugenini.
United vs South 5
United vs South 5
Kipigo cha leo kinaifanya Man United kuendelea kubaki nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, ikiwa na point 37 katika michezo 23. Huo ni mchezo 6 kwa Man United kupoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.
United vs South 4
United vs South 4
Vikosi vya timu zote vilivyocheza mchezo wa leo Manchester United vs Southampton
United vs South
United vs South
Takwimu za mchezo kati ya Manchester United vs Southampton
United vs South 1
United vs South 1
Matokeo ya mechi nyingine za EPL zilizopigwa leo Jumamosi January 23
Norwich 4-5 Liverpool
Crystal Palace 1-3 Tottenham
Leicester City 3-0 Stoke City
Man Utd 0-1 Southampton
Sunderland 1-1 Bournemouth
 Watford 2-1 Newcastle Utd
West Brom 0-0 Aston Villa

No comments: