Mahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi Inafanyiwa Kazi- Mwakyembe - LEKULE

Breaking

5 Jan 2016

Mahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi Inafanyiwa Kazi- Mwakyembe

WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia. 
Dk.Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi kwa karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli wakati wa kampeni. 
Mwakyembe amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni vyombo vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya kazi kwa wananchi kwa kutenda haki. 
Amesema kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya mtu mmoja. 
Mwakyembe amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’ majipu’katika tasnia ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo yatumbuliwe kabla ya Rais Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila sindano ya kupunguza maumivu (Ganzi). 
Mwakyembe amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali wanazokumbana nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha wanayoishi hivyo serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao. 

Mkurugenzi wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.

No comments: