COSOTA waja na hili kuhusu malipo ya wasanii - LEKULE

Breaking

15 Jan 2016

COSOTA waja na hili kuhusu malipo ya wasanii



Kuna utaratibu mpya ambao unakuja kuhusu wasanii wa muziki kulipwa baada ya nyimbo zao kuchezwa kwenye vituo vya TV na radio, wakati huohuo kuna neno mirabaha ambalo huenda umekutana nalo na hujajua maana yake na linahusiana na nini.
Hii ndio maana ya mirabaha iliyoelezwa na Doreen Anthony Sinare ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) >> ‘Ni kipato ambacho unakipata kutokana na kazi ambayo umeitengeneza… inawezekana umeuza nakala, unatafsiri kazi, umekodisha au kutangaza.. pesa unayoipata ndio mrabaha‘- Doreen Sinare.
DOREEN
Hapa imetajwa idadi ya wasanii wa muziki waliosajiliwa COSOTA mpaka sasa>>> ‘Kwa kukadiria ni kama 21% waliosajiliwa, mtaani kuna nyimbo nyingi lakini hawajisajili‘- Doreen Sinare.
Vipi kuhusu ishu ya vituo vya TV na Radio kulipia nyimbo za wasanii, haitashusha muziki wa TZ? >> ‘Kisheria inatakiwa muziki wa ndani upewe 60% hewani.. naamini muziki wetu ni mzuri, nadhani haitokuwa hivyo tunavyofikiria… siamini kama kituo kinaweza kumaliza siku bila kupiga wimbo wa ndani


No comments: