Hussein Bashe Amvaa Benard Membe Kwa Kumkosoa Rais Magufuli.......Amtuhumu Kutumia Safari Za Nje Kusafiri Na Hawara Zake! - LEKULE

Breaking

25 Jan 2016

Hussein Bashe Amvaa Benard Membe Kwa Kumkosoa Rais Magufuli.......Amtuhumu Kutumia Safari Za Nje Kusafiri Na Hawara Zake!


MBUNGE  wa  Nzega Mjini kwa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohammed  Bashe amejitokeza hadharani na kumtaka Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kulipotosha taifa kutokana kauli zake juu ya utendaji wa Rais John Magufuli.
 
Hivi karibuni, Membe alikosoa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Magufuli. Pia, alipinga hatua ya kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
 
==>Kupitia  ukurasa wake wa facebook, Bashe  ameandika;
 
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.
Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa au ndogo  ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekua sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi,.

Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake .Magufuli anaamini matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya nakuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu membe afahamu Magufuli ana style yake ,tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari.Membe kama yeye binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kulimuathiri yeye binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Commonwealth thats why leo anakosoa.

Tunafaham maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA  Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka katika Awamu ya nne, Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yeye amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekua mmoja wa mawaziri walioua foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu ya mis use of funds katika wizara yake, kipindi chake Bernad Membe safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathirika directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi. Aliwahi kusema Sankara " You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali 

Tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakua style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

No comments: