Hakuna atakayebomolewa nyumba aliyejenga katika umbali unaoruhusiwa kisheria -Kalua - LEKULE

Breaking

18 Jan 2016

Hakuna atakayebomolewa nyumba aliyejenga katika umbali unaoruhusiwa kisheria -Kalua


IMG_1034
Mbunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Bonnah Kalua akizungumza na vyombo vya habari.(Picha na Maktaba).

Na Skolastika Tweneshe-MAELEZO
Mbunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Bonnah Kalua amesema kuwa hakuna nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa katika umbali unaohitaji kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.
Mh.Kalua alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata kwenye mkutano wa hadhara.
Aidha alitoa wito kwa wale ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao zimewekewa X kujiorodhesha majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili wamfikishiea Ofisi kwake kwa ajili ya kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu na hatimaye wapate haki zao.
Mh.Bonna aliwatahadharisha wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha kwa kigezo cha kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia nzuri kwa wananchi kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa kwa niaba ya nchi nzima.
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko 

No comments: